Katiba

KATIBA YA W.A.G PROGRAM

MAELEKEZO
MWANZILISHI
A.Israel,Imani Shabani Dimanche ndiye mwanzilishi wa W.A.G Program, Anao uhamuzi juu ya shirika lake ao kampuni, Lakini Mkuu zaidi na kwakiasi kikubwa ni Mungu ambaye anastahili sifa na ukuu wake ni usio pimika. Zaburi 145:3-(4-17).
B.Mwanzilishi ana muhuri wa kampuni ao shirika na Coordinator ana muhuri wa Utendaji , Director ana muhuri wa center.SCUF,SLC na SED ni shirika zinazo simamia vitengo mbali mbali chini ya W.A.G.Program. Kipato cha shirika kita gawanywa kama ifuatavyo : Kampuni 37% na Shughuli nzima 63%.

C. Jamii ina maanisha: vyote katika umoja na katika utawala mmoja. Ikiwa wewe ni mwana memba wa jamii una hitajika kuleta utajiri wako wote bila kutafautisha kitu chochote. Kuna utafauti kati ya mwana memba na mfanya kazi. Ikiwa umehachana na uwanamemba hahiwezi kuzuru wewe kuwa kama mfanyakazi. Lakini utokapo kwa kosa lolote kama mwanamemba kutakuwepo na ukosefu wa amani kwako.

D. Ni katazo kuzungumzia kuusu mabadiliko ya katiba yanayohusu mwanzilishi katika mikutano yoyote ya shirika la W.A.G.PROGRAM, Baada ya mwanzilishi, hakuna awezaye kuwa presindeti ao mwenyekiti. Shirika litaendelea kuongozwa na Admin na Coordinator.

COORDINATOR

A.Huyu ni mwenye ujuzi wa kibyashara, na anawajibika na mikakati dhana na ushonaji wa kampeni kwa kuongeza kipato kwa ujumla na ufahari wa shirika inayo husu kazi na uchunguzi wa matokeo kwa kukamilisha mahitaji ya wa tangazaji na wauzuriaji na kushirikiana katika njia za ubunifu ambazo zitakazo rizisha maitaji na kuhamasisha shirika.

B.Coordinator anapashwa kutokea tu kwenye familia ya wahanzilishi, atakaye twaa na fasi hiyo ina bidi awe mwenye kujuwa ukweli wa neno la Mungu. Coordinator ana wajibika na utendaji wote kwajumla chini ya mwanzilishi na ana itajika kuripoti kwa mwanzilishi kabla ya uhamuzi wowote, anao uwezo wakuteuwa ao kuondowa mfanyakazi yeyote apatikanapo na kosa lolote liwezalo kuchukuliwa atuwa ya kuondolewa. Anawajibika kutetea ndugu na shirika kufuatana na maandiko matakatifu. Vilevile wanahitajika kutumia wanamemba kwa kutafuta ukweli ao uhakika wa makundi mengine na mahidara mbalimbali.

FACILITATOR
A.W.A.G PROGRAM Facilitator anatakiwa kuchaguliwa na familia ya wahanzilishi, wanatakika kiutendaji na wengine kama timu. Nao vilevile wana itajika kwa utetezi wa wandugu na shirika kufuatana na maandiko matakatifu.wana pashwa kutumia wananamemba kwa kutafuta ukweli na uhakika kwenye makundi na kwenye ma hidara mbalimbali.

B.Facilitator ni mkamilisaji katika shirika, anaitajika kutokea kwenye kundi na awe na uwezo wa kiutendaji..Wana itajika kushiriki katika makundi kwa suluhisho la matatizo ya shirika. Anahitajika kuripoti kwa Coordinator kabla ya uhamuzi wowote kuchukuliwa.

DIRECTOR
A.Director ni mtendaji wa uhundaji wa shuguli, haya majukumu ni yakukuza sura ya shirika, mipango na utu wa shirika kupitia matangazo ya usiano wa jumuhiya. Pia ana faa kuandaa na kutowa matangazo na mahuzurio kwenye vyombo vya habari na kwenye vipeperushi.anafaa ku towa mashindano mahalum na uhusiano wa umma wa mradi.

B.Director ana chaguliwa na familia ya uhanzilishi, wala hakuna uchaguzi , Ijapokuwa atakapo kuwa na tatizo yoyote inayo hitaji azabu, Facilitator na viongozi wa ma timu wana weza kuchunguza mambo zaidi kufuatana na imani. Director anaweza kubadilishwa na fasi yakazi ao kitengo ikiwa hakuna mahelewano kati yake na wafanyakazi.
ACCOUNTER
Na fasi hii ina sahidia maneja kwa kuendesha bihashara kwa operesheni ya malipo ya shirika. Ana faha kushugulikia Akaunti kupokea na kulipa bili na kulipa mishahara. Kazi hii piaikiwemo,kuhudumisha rikodi za benki,kwa utumiaji wa kila siku kwa wa meneja na kushugulika na bajeti ya shirika . naye pia uchaguliwa na familia ya uhanzilishi na awe mwaminifu.
AUDITOR
Nafasi hii ina chunguza kipato cha shirika njisi gani walivyo tumia kipato. Vile vile wana weza kuchunguza vitengo vingine na kutowa ripoti kwa Coordinator na kwenye Famili ya wahanzilishi.
Pia anachaguliwa na Familia ya uhanzilishi.
TEAM LEADER
Wana takiwa kutuma watu kutetea na kuhakikisha ukweli wa tatizo linapo tokea kwenye shirika,makundi, makampuni ao bihashara.
RULES
1.Kila Mtoto kwenye mpango huu anahaki ya kushiriki katika shuguli zote zinazo andaliwa na shirika kama vile Mafunzo ya Biblia: ili kujifunza neno la Mungu.
Mikutano ya Shirika: watoto ukusanyika wakati ukiwepo wageni ao wengineo wanao wahitaji.
2.Shirika hili lina sahidia watoto yatima na watoto maskini waliokuwa na umri wa miaka 3-16
Bila ubaguzi wa rangi,kabila,Luga,taifa ,ugeni, dini ao njisia yao.
3.Kila mwana memba na kila mfanyakazi anafaa kuwa mwaminifu na uwazi katika kazi kwa kuhonyesha upendo wao na msaada wao kwa wateja.
4.Director ana faa kupangilia afazali mkutano moja na wanamemba na wazazi wa watoto kila myezi mitatu.
5.Kuna wasaidizi wa kumsahidia Director kurikodi mipango shughuli zote, mabadiliko yoyote ya na faa kuripotiwa. Wasaidizi hao watakuwa kama watendaji ao wameneja kwenye ofisi ya Director.
6.Kununua ao kuhuza kitu chochote cha shirika , inabidi uhonyeshe resiti na maelezo, sababu na umuhimu wa kununua ao kuhuza(kuhuzisha) kitu hicho.
Vile Vile kwa njia ya ugawaji, inabidi kuonyesha form ya maelezo na sahni .
7.Center za W.A.G program zina weza kupokea wageni kutoka nafasi mbalimbali ya dunia. Kwa ustawi, Shirika litahitaji kwa wageni watakao uzuria kutuma baruwa kwa Coordinator kwa mpangilio na julisho kwa directors kwa tariki na center wanayo hitaji kuhuzuria.
8.Ni majukumu ya Directors kujulisha Facilitator kuusu mfanyakazi aliye ondolewa na kuchunguza kabla ya kuhajiri mfanyakazi mwingine badala ya aliye ondolewa.
9.Kila mtoto anafaa kujuwa jina la mfadhili wake na kufahamu namba yake.
10.Wafadhili wanaweza kuhachana na mtoto wakati wowote.
11.Kila mfanyakazi atakaye tumia vibaya fedha za shirika visivyo halali, anafaa kurudisha pesa hizo na 20%. Na kuchukuliwa hatua kwa matokeo kwa kutoheshimu utawala.
Banki Lambert itatumiwa kwa wale wanao chukuwa mikopo ku W.A.G.Program.
12.Wazazi wana haki ya kuhulizia kuhusu watoto wao kwa directors ao kati ya wafanya kazi wa shirika.
13.a)Mama ndiye anayo haki ya kupokea msaada wa mtoto kufuatana na kitabu cha (mwanzo 3:16) .

b)Kila mwana memba atakaye changa mchangowake kwenye W.A.G program hawezi kudai arudishiwe mchangowake wakati ahachapo mtoto ao atokapo kwenye shirika maana ni neema.
Katika shuguli zetu zote za kibiashara na za wafanyakazi wote wana pashwa kuongozwa na sheria za yesu Christo na mafunzo mengine matakatifu yatokayo kwenye agano Jipya na Agano lakale.)

Imani Shabani MWANZILISHI tena(ADMINISTRATOR)

Imani Pililo COORDINATOR tena (MTENDAJI)